TIBU VINDONDA VYAKULA NDUI KWA KUYUMIA ALOEVERA - PRINCESS HD TV

Breaking

Translate

Translate

Wednesday, July 3, 2019

TIBU VINDONDA VYAKULA NDUI KWA KUYUMIA ALOEVERA


 
Dawa ya vidonda vinavyotokana na Ndui ya kuku au vidonda vingine vyovyote:
》 Dalili ya Ndui 
_ Kuku hupata vipele vya mviringo kwenye upanga wake wa kichwani, kwenye masikio,miguuni na kwingineko kusikokuwa na manyoya.
》Kuandaa 
- Chukua majani ya Shubiri mwitu na kuyachana vipande vidogo vidogo. Vitwange na 
pumba kidogo na kuvianika. 
- Vikiisha kauka vitwange na kuchekecha upate unga laini. 
- Hifadhi unga katika chombo kisafi na kikavu.
》Kutumia 
- Safisha vidonda vilivyotokana na ndui au vidonda vyovyote vile na maji ya vugu vugu safi yaliyo na chumvi kiasi. 
- Pakaa unga wa Shubiri mwitu katika vidonda vilivyosafishwa. 
- Rudia baada ya siku moja. Tumia hivyo hadi vidonda vikauke. 
》NAMNA YA PILI YA KUANDAA DAWA HII
Shubiri mwitu  ukikata jani lake huwa linatoka utovu/maji maji ( angalia picha)
Baada ya kusafisha vidonda vya ndui na maji ya vuguvugu yenye chumvi kiasi na wakati huo unavisafisha hakikisha unavibandua.
》 Utachukua jani la shubiri mwitu na kulikata yale maji maji yatakayotoka utayadondoshea kwenye vidonda

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages