FAHAMU KUHUSU MBUZI BORA WA NYAMA - PRINCESS HD TV

Breaking

Translate

Translate

Saturday, July 20, 2019

FAHAMU KUHUSU MBUZI BORA WA NYAMA




ASILI

Kiasili ni mbuzi wa Afrika ya kusini ingawa ndani yake kuna damu toka baraUlaya na India, hii ndio Mbegu kubwa Zaidi ya mbuzi wa nyama ukilinganisha na wengine. Pia wanazalisha kiwango kikubwa cha maziwa ingawa wanafaa Zaidi kwa nyama.


RANGI
Wana mwili wenye rangi nyeupa na kichwani wana rangi nyekundu au hudhurungi (brown) ingawa wapo weupe kabisa au wekundu/hudhurungi kabisa na hii hutokea kwa 0.001%




UMBO
Wana umbo kubwa kufikia kilo 110-135kwa madume
Kilo 90-100 kwa majike
Wana masikio yaliyolala kama mbuzi wa kinubi (Nubians)


UZAZI
Huwa wanazaa mapacha na huweza kuzaa mara 2 kwa mwaka
Majike ni wazazi na walezi wazuri wa watoto sababu wana maziwa ya kutosha
Watoto hukua haraka sana, na nia aina ya mbuzi ambao sio wakorofi (docile)
Kwenye baridi kali au joto kali huwa inawaathiri kwenye kubeba mimba

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages