Zari amsikitia Tanasha kupewa ujauzito na Diamond Platnumz - PRINCESS HD TV

Breaking

Translate

Translate

Saturday, June 29, 2019

Zari amsikitia Tanasha kupewa ujauzito na Diamond Platnumz

           


Mjasiriamali , Zari The Bosslady amempongeza Tanasha kwa kupewa ujauzito wa Diamond Platnumz.

Hata hivyo licha ya pongezi hizo, amemsikitikia mrembo huyo wa Kenya, kwa kuwa amepewa ujauzito na baba wa watoto watatu asiyewajibika kama baba.

Kwenye video fupi iliyochukuliwa kwenye Insta live Ijumaa hii, akiwa Nairobi Kenya kwa mwaliko wa Akontee zari alisikika akisema "Kuna mtu anasema Tanasha ni mjamzito comment inakuja kila mara, ni vizuri kuwa mjamzito ni kitu kizuri lakini kitu kingine ni kuwa baba wa watoto watatu asiye wajibika kwahiyo inanifanya nihoji vipaumbele vyake kwahiyo hongera nina matumaini unafedha za kutosha benki kwaajili ya kumtunza mtoto huyu unajua kwasababu yuko hivyo alivyo."

Ijumaa hii Tanasha na Diamond walikuwa wakifanya photoshoot kwaajili  ya shughuli ya kifamilia iliyopangwa siku ya Sabasaba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages